23 Jul 2024 / 88 views
Hojbjerg kutua Marseille

Klabu ya Ufaransa ya Marseille iko kwenye mazungumzo ya juu ya kumsajili kiungo wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anaaminika kuwa tayari kuondoka kaskazini mwa London na anapatikana kwa takriban £17m. Majadiliano yanaendelea kuhusu masharti ya malipo, lakini pande zote mbili zinatarajia makubaliano hayo kutekelezwa.

Hojbjerg alijiunga na Spurs mnamo 2020 kwa dili la £15m kutoka Southampton, wakati Jose Mourinho alipokuwa kocha.

Aliichezea klabu hiyo mara 39 msimu uliopita lakini ni mechi 10 tu kati ya hizo alizocheza huku Ange Postecoglou akiwapendelea Yves Bissouma na Pape Matar Sarr katika safu ya kati.

Raia huyo wa Denmark ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Tottenham na atapatikana kwa uhamisho wa bure 2025 ikiwa masharti mapya hayatakubaliwa.

Spurs wameimarisha safu yao ya kiungo msimu huu wa joto kwa kuwasajili Archie Gray kutoka Leeds, na Lucas Bergvall kutoka klabu ya Djurgardens ya Uswidi.

Marseille wamekuwa kwenye harakati za kuajiri tangu kumteua meneja wa zamani wa Brighton Roberto de Zerbi.

Mshambulizi Mason Greenwood amejiunga kutoka Manchester United, na kiungo Ismael Kone alikamilisha uhamisho kutoka Watford mwezi huu. Pia wanadaiwa kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah.